Skip to content

Rais Jakaya Kikwete aiweka nchi rehani kumuokoa mwanae asinyongwe China.

September 7, 2012

Ningumu kuamini lakini ni UKWELI

 

Taarifa za upelelezi makosa ya jinai nchini China zinasema tarehe 01/7/2012, vijana wawili wenye asili ya kiafrika walikamatwa katika uwanja wa ndege wa  Hong Kong usiku, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi za Tanzania Bilioni nne, mkuu wa kitengo chakuzuia mihadarati cha uwanja wa Hong Kong  Yiu-Kwong anawataja kuwa ni Ridhiwani Jakaya Kikwete na Abdalah Aman Mohamed

 

Mnamo tarehe  2/7/2012 majira ya saa nne (4:13) za usiku hapa Tanzania, rais Jakaya Kikwete alipokea simu kutoka kwa mtanzania mmoja aitwae Philip Malmo ambae ni balozi wa Tanzania nchini China, Taarifa muhimu baada ya salamu ilikuwa ni Ridhiwani amekamatwa uwanja wa ndege wa Hong Kong na madawa ya KULEVYA,

 

Kwa haraka, rais akamuuliza vipi suala hili limeshafika hapo ubalozini? Akajibiwa hapana ni mimi na kaimu wangu tu ndie tumepata taarifa hii mda huu, bado hatujaliifanya lakiofisi, tunasubiri ushauri wako mheshimiwa.

 

Rais alikata simu huku hali yake usoni ikibadilika gafla, ilichukua kama dakika 20 hivi rais akiwa kimya hata kutikisa macho tu hatikisi, baadae akainua simu na kumpigia rais Hu Jintao  wa China, Waliongea kwa mda mrefu yapata dakika 40 hivi, na walikonekana kama hawakubaliana kitu fulani katika mazungumzo yao. Baadae simu ikakatwa,

 

Akampigia simu Malmo nakumwambia suala hili walifanye kwa siri kubwa asijue mtu yeyote, naaweke maandalizi yawe tayari yeye anajiandaa kuja kulimaliza, kasha akampigia tena simu Hu Jintao na walitumia dakika 16 tu akainuka nakusema, vijana, mwambie SD53 aandae ndege haraka kwa safari ya China,

 

Gari ya kirai namba T 435 CDR aina ya Landcruiser nyeusi iliingia nakuwabeba watu watatu akiwemo rais Jakaya kuelekea airport, kama dakika 13 ikafika airport, tayari ndege ilishaandaliwa na palikuwa na maafisa watatu, wote tuliingia katika ndege ile isipokuwa yule dereva wa gari ambae aligeza mjini, hiyo ilikwa sasa ni saa 7:43 za usiku.

 

Tarehe 3, majira ya saa nane za usiku kwa china, tulifika China, hakukuwa na aina ya mapokezi yoyote ya kiserikali, na baada ya kushuka tulimkuta Malmo na msaidizi wake wakitusubiri, Malmo alikuwa tayari ameshaandaa hoteli lakini kulingana na tukio lilivyo tulikubaliana tusilale na tukammwambia mheshimiwa rais amwambie Hu Jintao kuwa ameshafika. Rais alitekeleza hilo na baada ya dakika 15 maafisa watatu wa china walifika nakujitambulisha kuwa wenyeji wetu, wakatuchukua hadi alipo Hu Jintao katika moja ya ikulu ya Hong Kong,

 

Kikao chao kilichukua masaa  manne, na jambo kuu walilokuwa wanakubaliana ni mashariti ya kumuachia, Hu Jintao alihitaji jambo moja tu, kwamba nini serikali ya china itapata kwakumwachia huru Ridhiwani? Kilichomvutia Hu Jintao naakamua muachia Ridhwani ni ahadi ya makubaliano ya Rais Kikwete kuwa ataipa China fursa ya uwekezaji wakudumu kusini mwa Tanzania ambako kumegunduliwa mafuta, gesi, na makaa ya mawe.

 

Kwakuwa sera ya china kwa sasa ni “Now we are going to Africa”, ilisaidia sana kukubali ombi hilo la jk.

 

Majira ya saa 11 alfajiri kwa saa za china, Ridhiwani aliletwa akiwa katika gari dogo, nakupokelewa na jk huku wakikumbatiana wote WAKILIA. Jk na Jintao wote kwapamoja wakamuonya sana nakumwambia ameliaibisha taifa la Tanzania, lakini kwakujitetea akasema sio yeye, ila inawezekana yule kijana waliyesafiri wote kutoka Ethiopia ndie mwenye mzigo huo.

 

Majira ya saa 12 za asubuhi tukaondoka kurudi Tz.

 

Taarifa hii ni yakweli mimi nilikuwemo kwenye msafara huo,

 

Hutaki unaacha, hulazimishwi kuamini.

 

Source   ni mimi mwenyewe.

 

Advertisements

From → Uncategorized

39 Comments
 1. Lembris P. Lemilya Mollel permalink

  Mi ni member mzuri sana ndani ya mtandao wa kijamii (JamiiForums) na hakika baada ya kuona thread kama hii toka kwa member mwenzangu Janson bourne hakika nimeshtushwa sana na hili.
  Sikutegemea kuona taarifa hii kama kiongozi kama Jk angeweza kufanya haya aliyoyatenda ktk Nchi yetu!
  Hakika kwa mtazamo wangu wa kivyangu kabisa ni kwamba hakika kama ni kweli ametutenda hv huyu ni kwmb angestahili ashitakiwe kabla hata ya kumaliza muda wake wa uongozi aliyenaye hv sasa.

  Natamani leo hii ningesikia kama Jk amekamatwa na kupelekwa kwenye vyombo muhimu kwa kustakiwa kwa hili alilotutendea Watanzania. Ingekuwa leo hii ni mtoto wangu amekamatwa huko China kweli si angesaport haraka na angeshanyongwa huko? Sheria ya China ktk kosa kama lile ni moja tu ni kitanzi itakuhusu mwenye tukio na hapa mtoto wa rais amefanya Nchi kuwekwa rehani kumwokoa kwa kuwa babaye ni rais.
  Hili Mi imenichafua nafsi yangu na sijui ni nini kitakacho nirudishia Imani na hawa viongozi wa serikali tawala ya ccm.
  Hakika haya majanga ya serikali tawala itawaweka ktk wakati mgumu sana ktk nyakati hii ya Watanzania wanavyozidi kuingia ktk ulingo wa Demokrasia ya ukweli.

  Sina mengi ila hakika hili la Jk + mwanae imenigusa nafsi sana.
  Jf imepotelea mbali hbr hii lakini MUNGU ni mkubwa na hakika itakuja mitandao isiyoogopa na daima watasema haki kama hii.

  Aluta continue!

  • NTSC permalink

   Jamani inch inakwenda wapi, ndio kweli Kila mbuzi hula kwa urefu wa Kamba yake. Nguvu twawapa sisi, na urefu wa Kamba yetu ni kura zetu. Tunawapa ahadi tutakura kwa urefu wa kamba zetu.

   Mungu ibaraki TANZANIa na uwauwe mafisadi wote.
   AMINA

  • mmarekani permalink

   Jamani tutumie akili how can somebody do shit like this me totally boooosh you danm ass

  • mmarekani permalink

   Jamani tutumie akili how can somebody do shit like this men totally boooosh you danm ass

  • Alice Ashly permalink

   @ lembrice ndio maana wanasubili muda uishe waseme mstaafu mbona hata waziri nanihii alifanya ufisadi wakajifanya kumshauri ajiudhuru leo wanasema waziri mstaafu anaustaafu gani wanatuchezea hawa si wahaona sisi ni mapoyoyo poa tu kaka tutafika

  • I can understand the love of a father to his son. But this is why when you reach certain levels. Your family needs to be coached on how to behave right so as not to put your reputation or integrity at risk. Waafrica we dont think this is important this is why such things happen. I am glad the boy was not killed but will he not repeat? what else will we give away next time if it happens???

 2. Bwana Lembris naamini ya kuwa wewe ni msomi anayeweza kupambanua mambo. Haya ni propaganda za watu kutaka kutuangamiza ili wafanikiwe kimaisha. Na sijui lengo lao lakini ukweli ni kwamba hawa watu wanafanya kila liwezekanalo wamuangamize JK na hivyo waone kuwa ameshindwa. Ninaamini kuwa JK ni binadamu na Ridhwani ni binadamu pia na isitoshe yeye ni mtu mzima anaweza kufanya maamuzi yake binadamu bila kumuhuzisha baba yake. JK kama JK hawezi tena kumzuia au kumchunga asifanye chochote anachotaka kufanya.

  Bwana Lempris hizi ni vita vya kisiasa na kama wewe sio mwanasiasa unaweza kuamini haya kujiingiza kichwakichwa na kujikuta unafanaya maamuzi yasio na staha kabisa. Hivyo basi nakushauri huwe makini na hawa wanasiasa.

  Jambo la madawa ya kulevya kukutwa kwa mtoto wa kiongozi ni kitu kibwa sana cha kimataifa na ingweza kuivolve vyombo vingi vya habari. Je iweje yeye tu ndiyo chanzo cha habari hizi?

  Yeye amekuwa kwenye msafara wa raisi wa nchi na anaamua kuja kutoa siri za raisi je yeye tumemuweka wapi kimaadili kwa ajili ya kazi zake. Huyu anafaa? Nani asiyefanya makosa? Na ndiyo maana wafanyakazi wa rais ndiyo wasiri wake wakubwa na hivyo hawaruhusiwi kutoa siri yeyote ile ya rais, yeye katoa, tumweke kwenye kundi gani?

  Mwisho:

  Napenda kusema kuwa huyu mtoa taarifa hii ni mwongo na anatakiwa aondolewe kwenye kundi la wastaarabu, hata kama taarifa ni za kweli au si za kweli. Ni vyema tukatambua umuhimu wa kuhifadhi hadhi ya taifa letu kwa kutotoa siri zinazoweza haribu emage za taifa either kwa kukuzudia au kwa ukweli wenyewe. Rais ni nguzo ya Watz wote, anaweza akaleta mtafaruku na watu wakauana kuliko kitu kingne.

  Je huyu mtoa mada anatoa kwa manufaa ya nani? Nani kamuhonga atoe uchafu kama huu kwenye mtandao?

  Ni bora afunge mdomo wake.

 3. mwisho watanzania wamejua na sasa atawaeleza nn?

 4. Salum Juma permalink

  Pumbavu zako habari za kutengeneza wapelekee baba na mama yako

 5. Michael J. permalink

  Mimi nimeshapata ugonjwa wa moyo. Duh!

 6. Mkami permalink

  Ni uhuru wa kutoa mawazo, lakini kiukweli kusema maneno ya uongo kiasi hiki tena pengine kwa ajili ya maslahi ya kisiasa ni kutomtendea haki Rais wa nchi

 7. Mkami permalink

  Yaani mwandishi wa taarifa hii ni muongo wa kutupwa, tazama hapa anavyosema “Rais alikata simu huku hali yake usoni ikibadilika gafla, ilichukua kama dakika 20 hivi rais akiwa kimya hata kutikisa macho tu hatikisi, baadae akainua simu na kumpigia rais Hu Jintao wa China, Waliongea kwa mda mrefu yapata dakika 40 hivi, na walikonekana kama hawakubaliana kitu fulani katika mazungumzo yao”. Ina maana huyu mtu alikuwa akimuona Rais kweli mpaka aseme uso ukabadilika ghafla? jamani tumuogope Mungu, hakuna dhambi mbaya kama ya kusema uongo. Hebu angalia tena uongo huu “wote tuliingia katika ndege” Yeye kama nani wanaingia katika ndege?”

 8. Bob permalink

  nachelea kuamini

 9. barblando permalink

  jk c mwenzetu tena, hayo n machache 2 tunayo y jua, bt kuna maovu meng 2 y hawa ma fisad wa ccm ! jk hana busara wala hekima, namfananisha n kiongoz hasiye jielewa 2

 10. bill pierree permalink

  ebwana hii nchi imeoza pia nakupa hongera kwa kazi ngumu uliyoifanya na ya ujasiri hakika wewe ni mpiganaji japo pia ni hatari kwa maisha yako sijajua umjiandaaje maana huyu jamaa na mtandao wake anaweza akakufanya lolote endapo ataligundua hili kuwa limeleak

 11. John Mwadia permalink

  MIMI napenda kujua katika kuyaokoa Maisha Riziwani Mh. JK na mwenzake Rais wa China ni Makubaliano ya maneno tu ndio yalifanyika? ama kulikuwa na kusaini hayo makubalianoa kwa pande zote mbili?

 12. MMASSY permalink

  BADO WATANZANITA TUTANYAMAZA KIMYA TU

 13. Maselle permalink

  Rais hawezi kufanya hivyo hata kama ni mwanawe, naamini hawezi, kuna mambo mengine marahisi kuamua lakini si kama hilo , hapana napinga

  asante kwa taarifa,
  Rais wetu Mungu akusaidie sana, usije ukafanya kinyume na mapenzi yake yeye Mungu , uakajakupata shida.

  Tunakuombea

 14. Abunuwasi permalink

  Mzee Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

  WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.
  Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

  Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
  Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

  Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

  Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

  Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.

 15. Godfrey macha permalink

  Huyo dogo ni bora ange nyongwa coy amelisababishia hasara kubwa taifa kwa ajili ya maslai yao binafsi wange binafsisha nyumba yao ya msola

 16. Dismas haule permalink

  Ni jambo la kusikitisha kuona viongo tuliowapa madaraka wanayatumia vibaya,ni ngumu kuamini kama ulivyosema lakini haina jinsi ni dhahiri kwa maelezo yako uliyoyatoa ni ya kweli,naandika comment hii kwa machungu kuona ukoloni unarudi tena haswa Tanzania kwa kukosa viongozi wenye msimamona nchi yao

 17. peter permalink

  i am very very suprised by this, but still i have some questions 1. kwakuwa walio kuwa katika safari kwenda kumuokoa Ridhiwani walikuwa watatu yaani baba na maafisa wawili je, baada ya habari kama hii kutoka audhani kwamba raisi atajua aliye toa siri ni mmoja wapo kati ya ninyi wawili? naamini kama umeamu kutoa siri kubwa hivi utakua na vielelezo vyakutosha , hivyo kwanini usitumie fursa hiyo kulipeleka swala hili kwenye vyombo vya sheria ili uokoe Taifa lako dhidi ya Adui kama hawa na huo ndio Uzalendo wa kweli.

 18. JACQUE permalink

  HUU NI UONGOOO BABU KUBWAA, MLIONAJE GESTURES ZA RAIS WAKAT ANAONGEA NA SIMU EMBU ACHENI HIZOOOO

 19. JACQUE permalink

  NA HUYO ANAESEMA ALIKUWEPO CC TUNA UHAKIKA GANIII?

 20. we ni matako acha kutudanganya. wewe ni mlinzi wa rais ama mtoto wake au ndugu yake? yani tangu anapigiwa simu tena usiku, we ulikuwepo hadi ukaiona sura yake ikibadilika baada ya kupokea simu ile na pia ukajua alikuwa anaongea na Malmo, au aliweka loud speaker nawe ukasikia???
  Acha kutueleza habari zako za kutunga au unajifanya Willy Gamba nini? We umetumwa nini? Matumizi ya blogu sio kuandika habari za uongo aisee. Unaona utaaaaamu kutuandikia upuuzi wako huu na kujifanya ulikuwepo katika msafara.

  Nahisi ulikuwa umelewa wakati unaandika hizi pumba zako…

 21. Basa Ze great permalink

  inasikitisha sana kuipeleka nchi kuzimu kwa maslai ya wachache walioaminika na kusemwa kuwa wameshinda kwa kura nyingi za wananchi maskini. hakika Tanzania ya sasa imepoteza mwelekeo na imekuwa kama kituo cha watu kusubiri mateso kama ya Guantanamo.

 22. Aise kama tutaendelea kuzigawa rasilimali zetu kwa kulipa fidia! Ni wazi kuwa watanzania wachache watakao nufaika! Swali ni kwamba kwani ni watanzania wangapi wanaokamatwana kosa kama hilo na kuwajibishwa? Namna hiyo watoto wa vigogo wataendele na kazi hiyo huklu wakiendelea kuiweka nchi yetu lehan! Jaman tumepatwa!

 23. kato permalink

  hakuna shida mie nafikiri hata na jina la tz tulibadili tuwe kama kongo tuanze fresh kuwa mkataba waliingia tz na sio new country ndipo hapo vichwa vitawaka moto

 24. Dave permalink

  this is a just a drop in a sea..kuna mengi tu yamekwishafanyika na yakamalizwa kimyakimya.

 25. nuf permalink

  mbona story yako ni uongo mtupu,ukichambua unaona km ni kauchochezi fulani hivi

 26. Elimika ujue ukweli permalink

  Naomba uache kuandika uongo. Yani taarifa kama hii inaweza kumdanganya mtu ambaye hana akili lakini sio watu tulio soma.

  kwanza story yako haina ukweli kwanzia mwanzoni.

  Kwanza Hong Kong na China ni nchi mbili tofauti kabisa, zote zinatumia hela tofauti, serekali tofauti, mpaka lugha tofauti. Wachina wanaongea mandarin na wa hong kong wanaongea cantonese. Hong kong ni nchi ya kidemokrasia na china ni ya udikteta. sasa hapo unaposema mtoto wa raisi alikamatwa hong kong ndani ya china au kusema raisi aliongea na raisi wa china kusolve issue amabayo imetokea hong kong hai make sense kabisa.

  Ungeelewa jinsi wachina na wa hong kong wanavyochukiana usingechukua hata muda wa kukonect watu hawa wawili kwenye story moja.

  Kwahiyo sioni how Raisi wetu au mtoto wake wanaweza kufanya kosa katiba nchi mbili tofauti kwa wakati mmoja.’

  naomba next time ufanye research zaidi kabla ya kuandika uongo mbovu kama huu

 27. Alice Ashly permalink

  ndio maana maendeleo hakuna hivi kweli tutafika mbona uharibifu unafanywa na wakubwa na hawachukuliwi hatua yoyote tunaonyanyasika walalahoi watanzania tuamke hatutaki tena viongozi kama hawa wako kwa ajili ya manufaa yao tu hawana jipya .Huu ni ushenzi ningekua mimi mtoto wa masikini ningeshatupwa jla na kutangazwa na vyombo vyote vya habari kuwa ni muharifu …..Poa tu tutafika ipo siku watabainika

 28. muhande permalink

  Na wewe ni nani?
  Who exactly are you to be privy to such information? If this story is to be believed the source must be known. Otherwise it just sounds like well scripted anti-government propaganda. If noone else can collaborate your story publicly then it remains to be just that, a story, not fact.

 29. kama ni hali hii sioni hata umuhimu wa kupigia kelele ziwa nyasa a.k.a lake nyasa

 30. Haiiingii akilini,cm imipigwa alikuwepo!gari nyeusi nae yumo kwenye mkataba wa kumilikishwa gas ameona je ninani alitia saini? Angalieni taiga letu kupokea mane no juju itatu cost Sana tusiwe mavivu kufikiri nchi yetu no namba 1 Kwa majungu duniani

 31. Gabriel permalink

  Hiki ni kiama. Mungu atunusuru Watanzania. Pongezi kwa kuweka wazi. Kweli wewe ni jasiri sana.

 32. Kwa nini ni Lembris tu! ana comment kwenye thread za Osbourne!!?

 33. leticia permalink

  so ukiwa mtoto wa mwenye nchi unapeta!!
  but it’s to sad what about wengine ambao si watoto wa mapresident, jamani ila nijambo la aibu sana kwa taifa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: